"Hatima ya Yemen ni hatima ya Tehran," Israel yasema baada ya kuzuia kombora lililorushwa na Wahouthi

Israel imetishia kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Wahouthi la Ansar Allah nchini Yemen baada ya jeshi la Israel kulidungua kombora lililorushwa kutoka Yemen kuelekea Israel.

"Hatima ya Yemen ni hatima ya Tehran," Israel yasema baada ya kuzuia kombora lililorushwa na Wahouthi
Mfuasi wa Yemen wa kundi la Ansar Allah akiinua mfano wa kombora la "Palestine-2" katika mji mkuu, Sana'a.

Siku ya Jumamosi, Wahouthi walitangaza kuwa wamerusha "kombora la balistiki" kuelekea Israel "kujibu hatua za Israel dhidi ya Wapalestina katika vita katika Ukanda wa Gaza," kulingana na kundi la Yemen.

Kombora la Jumamosi lilikuwa la kwanza kurushwa na kundi hilo tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Iran mnamo Juni 24, kufuatia vita vya siku 12 kati yao.

"Mkono wake utakatwa"

"Hatima ya Yemen ni hatima ya Tehran," Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alisema katika taarifa yake. "Baada ya kupiga kichwa cha nyoka huko Tehran, tutawalenga Wahouthi huko Yemen pia. Yeyote atakayeinua mkono dhidi ya Israeli atakatwa mkono wake."

Israel inalitishia kundi la Ansar Allah kuwa italiwekea vikwazo vya majini na anga iwapo itaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Israel.